Header

Mose Iyobo adai hafikirii kuja kuwa muimbaji

Kuna madancer wengi ambao wameacha kazi hiyo na wameingia kwenye kuimba. Wapo wanaofanya vizuri na pia wapo ambao bado hawajafanikiwa kwenye upande wa kuimba. Tulitaka kujua kwa upande wa Mose Iyobo iwapo amewahi kutamani kuacha kudance na kuingia kwenye kuimba.

Amesema, “Kwa upande wangu mimi sijawahi kufikiria kuimba, nina uwezo wa kuimba kama vile nikimuona Simba anaimba naweza kumjaribisha, akina Harmonize naweza kuwajaribisha. Lakini sijawahi kufikiria eti niache dance na niimbe kwasababu naona sitokuja kuwa muimbaji mzuri. Na ukiacha na yote mimi sio muimbaji ila napenda kuimba. Tunaona wapo wengi wameacha kudance na kuimba lakini hawafiki popote wanaenda wanarudi, labda wanatakiwa kujitangaza zaidi.”

Miongoni mwa madancer waliowahi kujaribu bahati zao kwenye kuimba ni pamoja na Makomando, Msami na wengine.

Comments

comments

You may also like ...