Header

Ray: Mimi na Chuchu tunaandika caption kwenye akaunti ya Instagram ya Jaden kwa kusoma hisia zake!

Kwa sasa kuna tabia ambayo wazazi wengi wamekuwa wakiifanya kwa watoto wao kuwafungulia account za Instagram pindi tu wanapozawaliwa. Muigizaji wa filamu nchini, Vincent Kigosi aka Ray naye ni kati ya wazazi hao.

Hata hivyo watu wengi wamekuwa wakidiss kutokana na zile caption zinazoandikwa na wazazi hao, Ray na mchumba wake Chuchu Hansy. Leo ameamua kufunguka kuhusu issue hiyo.

“Unajua mtoto ni hisia, unapokuwa na mtoto unatakiwa kujua anakuwa anahisi nini. Kwa vile mtoto hawezi kuongea sio kwamba mimi au mama yake tunaamua tu kuandika vile hapana, isipokuwa tunasoma hisia zake kuanzia anapoamka mpaka usiku anapolala, tunajua anasema nini au anataka nini, ndo tunaandika, ndio maana tunasema mtoto ni hisia,” amesema.

“So kwa wale wanaotokwa na mapovu kwasababu naandika maneno tofauti na umri wake wafahamu tu wanaoandika ni wazazi wao kutokana na hisia tu tunazozipata juu yake,” ameiambia Dizzim Online.

Ray na Chuchu wamebahatika kupata mtoto kwa kiume aitwaye Jaden.

Comments

comments

You may also like ...