Header

Exclusive: Tuddy Thomas afanya wimbo na Diamond Platnumz kwenye ndege

Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania Tuddy Thomas ametoboa siri ya kazi za msanii Diamond Platnumz kuwa katika moja ya safari wakiwa kwenye ndege ilipatikana idea ya wimbo ambao ulirecordiwa ndani ya ndege mpaka mwisho kisha kumaliziwa walipofika mwisho wa safari.

Akizungumza na Dizizm Online producer Tuddy amesema kuwa katika album mbili ambazo Diamond tayari ameandaa upo wimbo ambao wazo lake lilipatikana kwa mzuka uliopanda wakiwa safarini kwenye ndege hali ambayo iliwasukuma kufanya kazi katika safari hiyo nzima ambapo Diamond aliandika mashairi na kurecordiwa sauti wimbo ambao ulimalizika walipofika hotelini.

“Ana nyimbo nyingi sometime uwa anapata mzuka kwenye ndege mimi napiga beat kwenye ndege pale namvalisha headphone tunakaa tunarecord, tukifika hotelini tunafanya final”

“Ana album mbili tayari kashafanya na ngoma iliyofanyika kwa mfumo huo wa kurecordiwa kwenye ndege ipo moja” Amesema Tuddy Thomas.

Hata hivyo Tuddy Thomas amekuwa mtayarishaji rasmi wa msanii Diamond Platnumz tangu mwaka 2012 hata kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kila wimbo ambao Diamond anapanga kuaachia.

“ukiaona hata kwenye akaunti yangu ya Instagram toka mwaka 2012 niliandika Diamond Platnumz official Producer it mean sasa hivi hawezi kuachia nyimbo lazima anishirikishe mimi na wimbo wowote ambao atakuwa naachia lazima mimi nipitie” Ameongeza Tuddy Thomas.

Comments

comments

You may also like ...