Header

Golden State Warriors wachukua ubingwa wa NBA

Timu ya Golden State Warriors imeitandika Cleveland Cavaliers na kuunyakua ubingwa wa ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani, NBA.

Warriors wameshinda michezo minne kati ya mitano ya fainali hizo.

Wameshinda vikapu 129-120 kwenye mchezo uliochezwa Jumatatu. Golden State waliwashinda Cleveland kwenye fainali za 2015 lakini wakaja kushindwa mwaka jana. Mchezaji wa Warriors, Kevin Durant, 28, ametajwa kama Most Valuable Player (MVP) wa fainali hizo.

“I couldn’t sleep for two days,” alisema Durant. “I was anxious, I was jittery. I just wanted to lay it all out there. I put in work, I just had to trust in it. We were really good tonight.”

Timu hizo mbili zimekutana kwenye fainali kwa mara ya tatu. Durant, aliyejiunga na timu hiyo akitokea Oklahoma City Thunder amekuwa na mchango mkubwa kwenye ubingwa huo.

Comments

comments

You may also like ...