Header

Kitambaa cha Asamoah Gyan na utata wake

Katika Mchezo wa jana wa kimataifa kati ya Ghana na Ethiopia, nahodha wa Ghana Asamoah Gyan alivaa kitambaa cha unahodha chenye picha ya sura yake, rangi ya bendera ya Ghana huku ikionekana pia namba 3 ambayo ni namba ya jezi yake ya timu ya Taifa.

Jambo hili lilipelekea Nahodha huyo wa Black Stars kuondoka na kitambaa hicho wakati akifanyiwa mabadiliko kumpisha Abdul Majeed Waris, kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mpira wa miguu kitambaa hicho ilibidi akabidhiwe nahodha msaidizi Andre Ayew ingawa Gyan aliondoka nacho na kupelekea Ayew apewe kingine kutoka kwa Kiongozi muwakilishi wa timu ya Ghana, jambo lililowashangaza mashabaiki wa soka na kuhisi huenda kukawa na chuki baina yao.

Baada ya Mchezo huo Asamoah Gyan allitolea ufafanuzi suala hilo na kueleza kuwa hakuna ugomvi baina ya wachezaji hao kama watu wanavozani.

“Nimekua kwenye timu ya taifa kabla ya Ayew, nimekua kama mfano kwake tangua aanze kuichezea timu ya Taifa. Baba yake alikua ananipenda sana”

“Kama Binadamu huwezi jua watu wanafikiria nini juu yako, kuna muda unaweza ukaniona na usinipende ni kitu cha kwaida tunaongelea uhalisia, lakini mimi navoona sisi hatuna tatizo lolote kama watu wanavoona”. Alisema Asamoah Gyan.

Katika mchezo huo Ghana chini ya kocha wao mpya Kwesi Appiah walishinda jumla ya magoli matano kwa sifuri dhidi ya Ethiopia huku Asamoah Gyan akifunga goli la kwanza na kukifikisha magoli 50 katika michezo yote aliyocheza timu hiyo tangu mwaka 2003 na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza timu hiyo kufikisha magoli 50.

 

 

Comments

comments

You may also like ...