Header

Lil Wayne amtukana Birdman live jukwaani

Lil Wayne na Birdman ni wakali ambao baada ya bifu lao lililodumu kwa takribana miaka miwili na nusu kisha majuzi kati kuonekana kama wamesawazisha mambo baada ya Lil Wayne kukutana na watoto wawili wa Birdman katika show na kupiga nao picha kisha picha hizo Birdman akazirepost kupitia ukuarasa wake wa Instagram amini mambo yamegeuka na kuwa katika sura nyingine.

Wikiend iliyopita akiwa kwenye tamasha katika show yake mjini Las Vegas, Lil Wayne katika hisia zake na joto la show yake hiyo kuonekana kuwa juu alirusha maneno ambayo moja kwa moja yalimlenga Birdman kwakuwa alimtaja kwa jina hali ambayo ilibayanisha kuwa wawili hao bado wako katika bifu zito.

Akiwa jukwaani kutoa burudani Lil Wayne alipaza sauti akifuata midondoko ya mdundo kwa kusema “Birdman, You Can Suck My D*ck” maneno ambayo yaliamsha kelele zaidi za walioudhuria show hiyo.

#lilwayne tells Birdman "YOU CAN SUCK MY D*CK" ….😳

A post shared by DJ Akademiks (@akadmiks) on

Hata hivyo Birdman wiki iliyopita kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha yake ya zamani akiwa na Lil Wayne kisha kuweka maneno ambaye hayakuonesha kuwa kuna tatizo kati yao ambapo mbali na kuwa Wayne ametumia maneno ya kumkosea heshima ambayo yanaaweka wazi kutokuwepo na maelewano Birdman hajajitokeza kuzungumza lolote.

 

Real Rap #gangsta music #cashmoneymillionaires #TB

A post shared by Birdman5star (@birdman5star) on

Comments

comments

You may also like ...