Header

Nilishindwa kuendelea kuwa na meneja anayetaka kuuza sura zaidi ya msanii – Becka Title

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Becka Title amesema aliamua kuachana na management yake ya zamani baada ya kugundua kuwa inamrudisha nyuma.

Ameiambia Dizzim Online, “kazi zangu zimelegalega kwasababu ya management, unajua zamani nilikuwa na management tukafanya kazi vizuri lakini mwisho wa siku hakuna kitu cha maana. Tumekuja kushindwana kwa vitu vidogo sana, unakuta meneja anataka ajulikane auze sura tu hakuna kazi inayofanyika, nikaona kabisa hapa tutashindwana, nikaachana nayo na ndio mpaka sasa hivi nipo mwenyewe bila management,” amesema.”

Aidha msanii huyo mwenye kipaji cha kipekee hakuacha kuzungumzia jinsi muziki ulivyobadilika kwa sasa.

“Muziki kiukweli umebadilika sana, ukiangalia wasanii wa hip hop zamani walikuwa wanaonekana wahuni, wakuimba walikuwa wanaonekana wastaarabu lakini kwa sasa hivi hamna kitu kama hicho, imeeleweka uhuni ni tabia ya mtu.”

Comments

comments

You may also like ...