Header

Nyandu Tozi adai ndoa haijamzuia kufanya muziki

Ndoa ni kheri lakini muda mwingine inasababisha mambo mengine kutoenda sawa ambapo wataalamu wamebainisha wivu ndio chanzo kikubwa. Rapper wa Micharazo, Nyandu Tozi ameelezea kwa upande wake ndoa inavyomwendea.

Ameiambia Dizzim Online kuwa hana tatizo na mke wake hata kidogo na mke wake haingiliani na kazi zake za muziki.

“Mimi ndoa haijazuia kazi zangu kwasababu sio mgeni kwenye masuala haya kwasababu kabla sijamuoa mke wangu nimeshaishi naye miaka mitano nyuma na tulikuwa tunaishi kwa system ile ile ya ndoa, Kwa sisi waislamu kama nimetimiza nguzo na matakwa ya dini. Lakini tofauti kwenye maisha yangu mke wangu hanizuii chochote kwenye muziki wangu, so ninapopata time nafanya muziki ninapopata time nafanya maisha yangu binafsi,” amesema.

Kwa upande mwingine huyo amewahakikisha mashabiki wa Micharazo kuwa kundi lao halina tofauti yoyote na soon kazi mpya inakuja.

Comments

comments

You may also like ...