Header

Tinashe adai Wamarekani Weusi hawajamkubali bado

Tinashe amesema kufanya muziki akiwa na mchanganyiko wa Uafrika na uzungu ni changamoto kubwa. Amedai kuwa bado hakubaliki na jamii ya Wamarekani Weusi. Pamoja na muziki kuwa mgumu kwa wengi, anaamini kuwa msichana mwenye mchanganyiko wa rangi ni changamoto nyingine.

“Kuna masuala ya rangi (colorism) yanayotokea kwenye jamii ya watu weusi ambayo yako wazi,” amesema Tinashe. “Ni kuhusu kujaribu kupata mlingano ambako nikiwa mwanamke aliyechanganyika, na wakati mwingine najihisi sifit kabisa kwenye jamii ya weusi, hawanikubali moja kwa moja, ingawa najiona kama mwanamke mweusi. Jambo hilo huchanganya wakati mwingine. Niko nilivyo.”

Licha ya kuchukuliwa na Janet Jackson kutumbuiza kwenye tamasha la kumbukumbu, kufungua ziara ya Nicki Minaj, Pinkprint na kufanya kazi na wasanii kama Chris Brownm Britney Spears na A$AP Rocky, Tinashe amesema anahisi kuwa tasnia ina nafasi kwa wasanii wachache tu wa kike.

“Kuna mamia ya rappers wa kiume ambao wanaonekana sawa, wanaoimba sawa, lakini kama ukiwa mwanamke mweusi, ni labda uwe Beyoncé au Rihanna. Ni ajabu sana.”

Hata hivyo muda mfupi baada ya mahojiano hayo, mashabiki walimshambulia kuwa anasingizia masuala ya rangi katika kufanya vibaya kimuziki. Mrembo huyo mwenye asili ya Denmark na Zimbabwe alitangaza kuachia album yake ya pili, Joyride ambayo hadi sasa mashabiki wanajiuliza lini itatoka.

Comments

comments

You may also like ...