Header

Uchaguzi TFF wawekwa bayana

Shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, imetangaza Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.

Akizungumzia mchakato mzima wa uchaguzi mbele ya waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli amesema kuwa, zoezi la kuchukua fomu na kuzirejesha ni Juni 16 mpaka 20, mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 hadi Juni 23.

Nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF, Makamu wa Raisi pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo kanda hzio zimegawanywa katika makundi kama ifuatavyo:  Mara na Mwanza, Shinyanga na Simiyu, Arusha na Manyara, Kigoma na Tabora, Katavi na Rukwa, Mbeya na Iringa, Njombe na Ruvuma, Lindi na Mtwara, Dodoma na Singida, Pwani na Morogoro, Kilimanjaro na Tanga na Dar es Salaam ambayo ni kanda pekee.

Mpaka mchakato wa uchaguzi unapoanza, Uongozi wa sasa wa TFF chini ya Raisi Jamali Malinzi ulioanza kazi yake mwaka 2013 utaendelea kuwa madarakani mpaka mchakato mzima wa uchaguzi utakapokamilika.

Comments

comments

You may also like ...