Header

Diamond kufanya show yake mwenyewe kubwa na ya kwanza London, Dec 17

Baada ya kuahirishwa mara mbili kwa show yake na Ne-Yo nchini Uingereza, Diamond anatarajia kutumbuiza show yake mwenyewe, kubwa na ya kwanza katika mji mkuu, London. Show hiyo itafanyika katika ukumbi wa THE O2 Indigo.

Amethibitisha Jumanne hii kupitia Instagram,” LONDON!!! UK!! UNITED KINGDOM!!! IT’S OFFICIALLY CONFIRMED THAT PLATNUMZ DIAMOND WILL BE ROCKING YOU ON THE 17TH DEC 2017 AT THE O2 INDIGO !!! Please tag my all uk fans!!!…EUROPE!!! LET’S GO TO LONDON ON THE 17TH DEC 2017….. !!!.”

Naye meneja wake Sallam amesema kwenye show hiyo Diamond atatumbuiza mwenyewe kwa masaa matatu.

“ONE MAN SHOW… 3 HOURS NON STOP. #DiamondPlatnumz #London #December17 #O2Indigo,” ameandika Sallam.

Pamoja na show hiyo, Diamond ametangaza zingine tatu mwezi ujao ikiwemo ya Goma, Congo, Kigali, Rwanda na nyingine Dar.

Comments

comments

You may also like ...