Header

Mayanga atangaza kikosi kuelekea COSAFA

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga, hii leo Juni 14, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 22 watakaounda kikosi kinachokwenda kuwania Kombe la Castle Cosafa nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars, inatarajia kuanza kambi rasmi Jumapili Juni 18, mwaka huu katika Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Taifa Stars inajiandaa na michuano ya Cosafa inayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu, Michuano hiyo inaandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika ambako Tanzania kama mwanachama wa Cecafa imepata mwaliko kushiriki.

Tanzania imepangwa kundi A pamoja na wapinzani wake Mauritius, Malawi pamoja na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.

kikosi hicho kilichotangazwa leo kinaundwa na;

Golikipa: Aishi Salum Manula, Benno David Kakolanya na Said Mohammed Said.

Walinzi ni Shomari Salum Kapombe, Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’, Gadiel Michael, Amim Abdulkarim, Erasto Nyoni, Salim Hassan Abdallah, Abdi Banda na Nurdin Chona.

Viungo ni Himid Mao, Salmin Hoza, Mzamiru Yassin Selembe, Simon Happygod Msuva, Raphael Daudi na Shizza Ramadhani Kichuya.

Katika safu ya ushambuliaji yupo Thomas Emmanuel Ulimwengu, Mbaraka Abeid Yusufu, Stamili Mbonde, Elius Maguli pamoja na Shabani Idd Chilunda.

Comments

comments

You may also like ...