Header

Ratiba Ligi kuu England yatangazwa

Ratiba kamili ya Ligi kuu nchini Uingereza 2017/2018 imetolewa rasmi hii leo, Ligi hiyo itaanza Agosti 12 mwaka huu katika viwanja tofauti nchini humo.

Katika ratiba hiyo siku ya kwanza itapigwa michezo kumi, Mabingwa watetezi wa taji hilo Chelsea wataanzia nyumbani kuwakaribisha Burnley ikiwa ni safari yao katika kutetea ubingwa huo. Manchester United na Arsenal ni miongoni mwa timu zitakazoanzia nyumbani katika harakati za kutafuta ubingwa.

Wapenzi wa soka watalazimika kusubiri mpaka desemba 9 ambapo ‘Manchester derby’ itapigwa, mchezo kati ya Manchester United na Manchester City katika uwanja wa Old Traford huku siku hiyo hiyo kukiwa na ‘Merseyside derby’ kati ya Liverpool na Everton.

Timu zilizopanda daraja ikiwemo Newcastle ambao ni mabingwa wa ligi daraja la kwanza watacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Totenham Hotspurs huku Brighton wakianzia nyumbani dhidi ya Manchester City na Huddersfield dhidi ya Crystal Palace.

Comments

comments

You may also like ...