Header

Saida Karoli azingatia mambo haya kwenye wimbo mpya wa ‘Orugambo’

Msanii wa muziki wa asili kutoka Tanzania ‘Saida Karoli’katika kuendeleza ukongwe wake wa miaka 15 katika kazi ya muziki, amepata motisha kubwa ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na kurudi na kazi mpya inayokwenda kwa jina ‘Orugambo’ neno linalomaanisha ‘Maneno maneno’.

Orugambo ni kazi ambayo imechezwa kwa kuzingatia miondoko ya Saida ya asilia ikiwa na michanganyika wa usasa chini ya utayarishaji wa Tuddy Thomas ambapo katika kutumia baadhi ya mawazo katika uandishi na melody ya wimbo huo Saida aliiambia Dizzim Online kuwa ametumia mawazo ya baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva waliowahi kutumia mawazo yake kama ishara ya kurudisha fadhira za kilichofanyika kwa kila aliyevutiwa na kutumia mawazo ya nyimbo zake za kipindi cha nyuma katika nyimbo zao.

Saida ameachia video ya wimbo wake huo mpya chini ya uongozaji wa Hanscana ambapo katika video ya wimbo huo Saida ameonekana akiendeleza utambulisho wake wa kupiga na kucheza ngoma utambulisho ambao amehaidi kuuendeleza siku zote.

Hata hivyo Wasanii wa kizazi kipya cha Bongo Fleva baadhi walioonekana kutumia mawazo ya nyimbo za Saida ni pamoja na Diamond Platnumz, Darassa, Belle 9 na wengineo.

 

Comments

comments

You may also like ...