Header

Stone Bwoy pingu kumhusu wiki hii

Staa wa muziki kutoka nchini Ghana aliye-shine zaidi na ngoma yake ya ‘GO HIGHER’ ‘Livingstone Etse Satekla’ a.k.a Stone Bwoy imethibitika kuwa wiki hii kuna kitu kikubwa kitatokea katika maisha yake.

Dr Louisa Ansong

Kupitia picha inayozidi kusambaa zaidi mtadaoni inayomhusu Stone kionesha kadi ambayo ni ya mualiko wa harusi yake na mpenzi wake Dr Louisa Ansong iliyopangwa kufanyika tarehe 16 siku ya Ijumaa ya wiki hii.

Kadi ya Mualiko wa ndoa ya Stone Bwoy na Dr Louisa Ansong

 

Kadi hiyo ya mualiko haikubainisha ukumbu wala eneo rasmi la tukio la kufungwa kwa ndoa ya wawili litakapo fanyika ambapo mbali na kuwa imeonekan wawili hao watafunga ndoa lakini bado imewashangaza wengi kwakuwa hawakuwahi kuona dalili za wawili hao kuwa katika mahusiano.

Hata hivyo kwa mwenendo wa taarifa za harusi hiyo imeonekana kuwa harusi ya Stone na Dr Louisa Ansong itakayofungwa siku ya Ijumaa itakuwa ni ya siri na tukio hilo litashuhudiwa na wageni waalikwa pekee.

Comments

comments

You may also like ...