Header

Video: ‘Speech’ ya Kimombo ya Ray Vanny kwenye mkutano wa waandishi wa habari Coke Studio yampaisha

Ray Vanny anazidi kupaa juu kwa kasi ya roketi. Mwaka huu ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki aliyetajwa kuwania tuzo za BET lakini pia alipata fursa ya kutumbuiza na staa wa Marekani, Jason Derulo kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Afrika.

Mwishoni mwa wiki, kulifanyika mkutano wa waandishi wa habari uliohusisha baadhi ya wasanii waliopo kwenye msimu huu pamoja na Jason Derulo. Ray Vanny alipewa nafasi ya kuzungumza na alipojimbulisha kuwa ndiye msanii pekee wa EA aliyetajwa kuwania tuzo za BET, ukumbi mzima ulimshangilia.

Wengi wamesifia uwezo wake wa kuzungumza Kiingereza, lugha ambayo ni mtihani kwa wasanii wengi wa Tanzania. “Go bro, we will vote 4 you & thanks 4 representing E.A to the world. Plus ur English is on point,” ameandika shabiki mmoja.

Mwingine ameandika, “I never thought Rayvany could speak this nicy,that’s much better than his brothers at WCB,#ipicrayvanny.”

Comments

comments

You may also like ...