Header

Abidal arejea Barcelona

Klabu ya soka ya Barcelona imemtangaza Beki mkongwe wa klabu hiyo, Erick Abidal kuwa Balozi rasmi wa klabu hiyo kuanzia mwaka huu.

Abidal,37 ameitumikia klabu hiyo kwa kipindi cha miaka sita akicheza zaidi ya michezo 200 tangu alipotua klabuni hapo akitokea katika klabu ya Lyon ya nchini Ufaransa mwaka 2007 akishinda zaidi ya makombe 15.

Abidal anaungana na mabalozi wengine ambao ni Rolnadinho Gaucho, Juliano Belletti pamoja na Rivaldo wote wakiwa wamewai kuitumikia klabu hiyo miaka ya nyuma.

Mfaransa huyo anakumbukwa sana na mamilioni ya wapenzi wa soka duniani baada ya kupona ugonjwa wa kansa ya Ini mwaka 2011 kabla hajarejea kucheza tena soka la ushindani.

Abidal arilejea uwanjani mwaka 2011 baada ya kusumbuliwa na Kansa ya ini

 

Comments

comments

You may also like ...