Header

Mayweather kurejea ulingoni na McGregor

Dec 28, 2015; Phoenix, AZ, USA; Cleveland Cavaliers forward LeBron James (23) and center Tristan Thompson (13) against the Phoenix Suns at Talking Stick Resort Arena. The Cavaliers defeated the Suns 101-97. Mandatory Credit: Mark J. Rebilas-USA TODAY Sports ORG XMIT: USATSI-232226 ORIG FILE ID: 20160509_mjr_su5_068.JPG

Bondia Floyd Mayweather atapigana na bingwa wa UFC, Conor McGregor katika pambano la uzito wa kati lililopangwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu mjini  Las Vegas nchini Marekani.

Mayweather, 40 amethibitisha pambalo hilo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Twitter akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo huku mpinzani wake ambae ni McGregor, 28 akiandika “The fight is on” ikiwa na maana pambalo lipo tayari.

Katika pambano hilo, inaripotiwa kuwa huenda kila bondia akapata zaidi ya Dola za kimareka Milioni 100 sawa na paundi Milioni 78.4 pesa ambazo ni nyingi katika historia ya masumbwi.

Mayweather anarejea tena ulingoni kupigana na Conor McGregor tangu alipotangaza kustaafu mchezo huo kwa mara ya pili baada ya kushinda pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao mwaka 2015. Katika mapambano 49 aliyocheza Mayweather hajapoteza pambano lolote huku McGregor akipoteza mapambano 3 kati ya 24 aliyocheza.

Comments

comments

You may also like ...