Header

Simba yaimarisha kikosi chake kwa Ngome ya Mbao

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imeendelea na hatua zake za kuwasainisha mikataba wachezaji kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa VPL pamoja na mashindano ya kimataifa yaani CAF Confederation Cup.

Kufikia sasa uongozi wa Simba umemtambulisha mlinda mlango wa Mbao FC Emanuel Elius Mseja baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Katika Klabu ya wekundu bado muendelezo wa usajili unamkaribisha Aishi Manula ambaye pia ameshasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Vile vile usajili wa walinda mlango hao kunaifanya Simba iongeze nguvu ya kuwa na idadi ya walinda mlango watano ambao ni Daniel Agyei, Peter Manyika, Denis Richard, Aishi Manula pamoja na Emanuel Elius Mseja.

Comments

comments

You may also like ...