Header

Akiba ya 50 Cent kutumika kwenye ‘Happy Death Day’

Kampuni ya Universal Pictures na Blumhouse wameachia rasmi trailer ya filamu ya kutisha ya ‘Happy Death Day’ iliyoandikwa na kuongozwa na staa mahiri wa filamu ‘Christopher Landon’.

Filamu hiyo inayotegemewa kuachiwa rasmi tarehe 13 mwezi Octoba mwaka huu ambapo mbali na wakali wengine kuhusika zaidi imemshirikisha Staa wa filamu za kutisha ‘Jessica Rothe.’

Hata hivyo katika Trailer ya filamu hiyo inaonesha wazi rapa 50 Cent amekula shavu la aina yake kwasababu ngoma yake ya ‘In da Club’ iliyotoka mwaka 2003 imetumika kwa kiasi kikubwa.

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...