Header

Hii ni siku ya heshima na kumbukumbu kwa TuPac Shakur

Tupac Shakur a.k.a 2 Pac amekumbukwa iku ya leo kwakuwa kama angekuwa hai leo angesherehekea kutimiza umri wa miaka 46 huku ikikubukwa zaidi kuuwawa kwake mnamo mwaka 1996.

TuPac inatajwa kuwa alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi tano ambapo aliumia sana kisha kupona ambapo baada ya kupona kwake aliingia katika kesi ya tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia ambapo alipatikana kuwa na makosa na kufungwa jela hatua ambayo tukio kubwa lililofuata kubwa baada ya maisha ya jela ni kupigwa risasi njiani akitoka kushuhudia pambano la bondia Mike Tyson na Bruce Seldon ambapo siku saba baadae alifariki akiwa ni mwenye umri wa miaka 26.

Hata hivyo maisha ya TuPac yanatajwa kuwa na mikosi wa kuishi jela kwakuwa Mama yake mzazi ‘Afeni Shakur’ akiwa na ujauzito wake alifungwa jela kwa tuhuma za ulipuaji mabomu na pia TuPac mwenyewe katika maisha ya ukorofi aliyokuwa nayo alionja mkono wa sheria kwakuwa alifungwa jela.

Comments

comments

You may also like ...