Header

Kalapina ahusisha mafunzo aliyonayo kama angetekwa kama Roma

Rapa na mwanaharakati wa vita dhidi ya biashara na matumizi ya madawa ya kulevya kutoka Tanzania ‘Kalapina’ amezungumzia ambacho angekifanya kama tukio la utekaji lililomtokea rapa Roma Mkatoliki lingetokea kwake.

Akizungumza na Xxl ya Clouds Fm, Kalapina amesema kuwa kama tukio hilo la utekwaji lingemtokea yeye kwa mafunzo aliyonayo isingekuwa rahisi kwa watekaji kwakuwa anagejitetea kiasi ambacho pengine isingewezekana kutekwa.

“Unapojipanga kutaka kum-provoke Pina unajiuliza mara mbili mbili, tunge-provoke-ana hapo ningeweza kutekwa labda nikiwa maiti nisingetoka nikiwa niko hai kwasababu tungezinguana labda wao wana mikwaju wangeichomoa lakini tayari wao nao mmoja, wawili watatu wangekuwa washalala ujue kwasababu kiukweli mafunzo ninayo na nimespend muda mwingi kujiweka sawa sawa” Alisema Kalapina.

Kalapina baada ya kimya cha muda jana rasmi ameachia ujio wa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Demu ni mkali’ aliyomshirikisha hitmaker wa ngoma ya ‘Mtoto wa kike’ chini ya utayarishaji wa mkongwe na mtayarishaji ‘Dunga’.

Comments

comments

You may also like ...