Header

Msanii ukitaka kukosana na management ulizia masuala ya hela – 20 Percent

20 Percent amekuwa na ukimya mwingi hali iliyotulazimu kumtafuta kutaka kujua umesababishwa na nini. Ameyataja makosa ambayo anaamini yamechangia kutokea kwa hali hiyo.

“Mi nafikiri kosa kubwa nililofanya ni kuulizia haki, maslahi na mantiki ya kazi yangu,” ameiambia Dizzim Online. “Hilo ndilo kosa kubwa ambalo nafikiri ni wasanii wengi wa kibongo wanalifanya. Yaani inapofikia hatua ya kuulizia unapataje pesa au unaingizaje pesa au pesa yako iko wapi hapo ndio utakapoanza kukosea, Katika muziki wa kibongo yaani unatakiwa ufanye kazi tu usiulize kitu chochote,” ameongeza msanii huyo aliyewahi kushinda tuzo tano mfululizo.

Percent amesema licha ya kuwa na nyimbo katika studio za Combination Sounds, hasimimawi tena Man Walter.

Comments

comments

You may also like ...