Header

Wema Sepetu kusomewa maelezo ya awali ya tuhuma za Madawa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, inatarajia kumsomea maelezo ya awali mrembo na staa wa filamu Tanzania Wema Sepetu na wenzake wawili, Julai 10, mwaka huu kwenye kesi inayowakabili ya kukutwa na msokoto mmoja na vipisi kadhaa vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kesi hiyo ya Wema na wenzake, Angelina Msigwa na Matrida Abas walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa mawili likiwamo la kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya.

Hata hivyo wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde, alidai mahakamani hapo siku ya terehe 14(Jumatanao) mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

 

 

 

 

Chanzo: Mtanzania

Comments

comments

You may also like ...