Header

Kendrick Lamar leo yake ni miaka 30 iliyopita

Rapa kutoka Marekani Kendrick Lamar ni mkali ambaye anazungumziwa zaidi na kutajwa katika malinganisho na wakali wengine wa muziki wa hip hop/rap ambao baadhi yao wameshaingia katika orodha ya ukongwe ambapo pia juzi kati ilithibitika kuwa atasikika kwenye album ya The Game mpya na ya mwisho ya ‘West Side Story.’

Kendrick ambaye amevunja record ya mauzo ya Platnum kupitia album yake ya DAMN ndani ya wiki tatu pekee, siku ya leo anasherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ambapo ametimiza umri wa miaka 30.

Hata hivyo Kendrick Lamar kutokana na umahiri wake wa michano na uandishi anaozidi kuonesha kila anapofanya ujio mpya, ameshatajwa na rapa Wale kuwa rapa bora kwake hata kusema kuwa marapa wachanaji hawamuwezi huku akimtaja Eminem kuwa rapa ambaye anaweza kumpambanisha naye.

 

Comments

comments

You may also like ...