Header

Timbulo afunga ukurasa wa kiki na kufungua ukurasa huu

Msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye ngoma mpya iliyotayarishwa na producer Mr. T Touch ‘Ndotoni’ Timbulo, amebainisha malengo ya lengo ya kasi na mfumo wake wa bandika bandua katika utoaji wa ngoma kwa sasa tofauti na kipindi cha nyuma.

Timbulo ambaye ndani ya inahesabika kuwa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana mpaka sasa meachia ngoma tatu amesema kuwa malengo yake ni kuzungumziwa zaidi kwa kazi zake na sio skendo na habari tofauti ambazo anaamini hazina tija kwenye muziki wake.

“Malengo ni kuwa na nyimbo atleast ni kuwa na nyimbo tano kwa mwaka, zikipungua sana basi nne na toka Mwaka umeanza hii ni realease yangu ya pili na ya tatu ni kolabo nilishirikishwa na Meda Classic …tayari tuna nusu ya mwaka alafu muda uliobaki naona kama bado ni mchache na nia ni ku-realease ngoma tano kwa mwaka” Alisema Timbulo akipiga stori na E Newz ya EA Tv.

Hata hivyo Timbulo ameonesha kufuata mfumo huo kwakuwa kasi ya muziki na wasanii wanaofanya vizuri katika kiwanda cha Bongo fleva iko juu sana kiasi ambacho sio rahisi kwenda nao sawa kama hautakuwa na kazi za kutosha hasa zenye ubora na uzuri kwa mashabiki.

Comments

comments

You may also like ...