Header

Bifu ya Davido na Wizkid yarudi tena, warushiana vijembe mtandaoni

Mahasimu wa Nigeria waliowahi kupatana, wamerudisha tena moto wa bifu yao. Wizkid na Davido wameingia kwenye vita vya maneno mtandaoni. Alianza Davido kwa kutupa jiwe gizani Jumamosi hii kupitia Snapchat. Dongo limedaiwa kuiponda EP ijayo ya Wizkid, ‘Sounds From The Other Side itakayotoka July.

Wizkid alijibu kimafumbo pia kupitia Twitter kwa kumwambia Davido asiwe na chuki kwa mtu anayefanya vizuri katika kile alichokishwa.

“U can’t hate on someone doing better than u in what u failed at! Learn and appreciate! Free ur mind from hate young kids 🙏🏾,” alitweet.

“The game is only for the real! Catch up or stay local! Don’t blame anybody for ur failures! Pray and work hard kids!,” aliongeza.

Baada ya kusaini na Sony Music, Davido alianzisha safari ya kimataifa ambayo haijawa na mafanikio. Hali hiyo imemfanya arudishe nguvu yake Afrika na amefanikiwa sana baada ya kuachia hits mbili, If na Fall.

Kwa upande wa Wizkid lakini, ameendelea kufanikiwa sana kimataifa na na hakuna ubishi kuwa ndiye msanii mkubwa zaidi kutoka Afrika kwa sasa. Katika kipindi cha mwaka mmoja tu, Wizkid ameshirikishwa na kushirikisha wasanii wakubwa wa Marekani wakiwemo Drake, Chris Brown na wengine.

Comments

comments

You may also like ...