Header

Moyo wa Gigy Money washindwa kusukuma damu pekee

Msanii wa muziki na Video vixen maarufu kutoka Tanzania Gift Stanford a.k.a Gigy Money amepindisha alichokisema kuhusu kuingia na kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote baada ya kuachana.

Ni muda wa wiki tatu sasa tangu Gigy ameimabia Dizzim Online kuwa hayuko tayari kuingia tena katika mahusiano hata kusema kuwa atakuwa single kwa muda mrefu zaidi kwasababu za kutotaka mahusiano yasiingiliane katika biashara na ndoto zake.

“niko single kwa muda mrefu kidogo, sihitaji mahusiano na sidhani kama Gigy Money anafaa kuwa na mahusiano kwasababu kwenye kipindi nina mahusiano hata hapa Dizzim nilikuwa siwezi kuja. Muda wote mimi nawaza Baby atakula nini…Baby atanionaje leo…kwanza mahusiano yanamfaa mtu ambaye tayari amemaliza goals zake…” Alisema Gigy Money.

Lakini kwa Gigy moyo wake ukakijikuta katika majukumu zaidi ya kusukuma damu ambapo usiku wa tarehe 6 Mwezi huu wa June kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwatakia mashabiki wake usiku mwema kwa picha ya Mo Jay huku akiambatanisha maneno yanayomaanisha kuwa amerudi rasmi tena katika mapenzi na Mtangazaji huyo wa Redio na picha nyingine tofauti hata zile ambazo wako pamoja zilifuata kwa kupokezana katika akaunti yake.

Good night my love❤️ AkA baba mwenye nyumba❤️

A post shared by ❤️FOREVER OG🙏🏾 (@gigy_money_og) on

Wakati mashabiki hajapata jibu sahihi kuhusu Gigy kurudi kwa Mo, siku ya Ijumaa kupitia FNL ya EATV/EA Radio Gigy alithibitisha kurudi katika amhusiano ambapo naneno yalimtoka kwa ishara ya kuonesha kuwa amezama tena mapenzi.

mnajiuliza kwanini ananipenda 😂 siri ya mtungi aijuae kata 😂

A post shared by ❤️FOREVER OG🙏🏾 (@gigy_money_og) on

“mimi niseme ukweli nampenda sana kwasabu kuna vitu ambavyo mtu ukimwambia hivi mwingine hivi kama sinema lakini mimi nakuta lakini namwambia it’s ok let’s go…kuna vitu mtu tu wa kawaida kumuacha hivi kama kumfumania…honestly mimi ndo nimempenda na sio kwamba jana au juzi…nilishakutana naye kama miaka minne sasa…Naishi naye na nina Tatoo yake” Alisema Gigy Money.

Comments

comments

You may also like ...