Header

“Nilifungwa pingu nikapelekwa kituoni” – Saida Karoli

Msanii wa muziki wa asili kutoka Tanzania mwenye ujio wa ngoma ya ‘Orugambo’ Saida Karoli amesimulia kipindi ambacho hakusikika alijikuta mikononi mwa polisi katika moja ya shows ambayo alihisiwa kuwa anaigiza sauti na kujiita Saida Karoli kwa kwa nia ya ulaghai.

Tukio hilo lilitokea Tabora katika hali ya kutomtambua kulingana alivyokuwa amelegalega kimaisha Saida amesema kuwa waliomtuhumu kwa ulaghai walimfikisha kituo cha polisi akiwa ni mwenye pingu mikononi ambapo alifanikiwa kuachiwa huru mara baada ya kujitete kwa mkuu wa kituo wa kipindi hicho aliyefanikiwa kumtabua.

“Kipindi ambacho nilikuwa kimya, changamoto ya kwanza ni ile ambayo nilienda ku-perform nikakamatwa wakasema sio Saida Karoli ni mwandada anaigiza…nikafungwa pingu nikapelekwa kituoni”

“Ilikuwa ni Tabora, yaani watu waliungana wengi wakisema sio yeye…yule ana hela, atafananaje hivi mazingira ya hivi hawezi kuja lakini nikajitetea pale mkuu wa kituo akanielewa akawaelewesha watu wakaniacha lakini wakati huo show imeshaharibika” Alisimulia Saida kupitia Capital Fm Tanzania.

Hata hivyo Saida tukio hilo aliliona kama moja ya changamoto katika safari yake ya maisha ya muziki kitu ambacho amesimulia kuwa ni hali iliyomtoa machozi kila wakati.

Comments

comments

You may also like ...