Header

Bonge la Nyau: Ukimya wa Alikiba utamletea madhara

Bonge la Nyau ameuzungumzia ukimya wa swahiba wake Alikiba. Akiongea na Dizzim Online, rapper huyo amesema ukimya wa Kiba una faida na hasara.

“Unajua Alikiba ni rafiki yangu, namjua sana tu,” amesema Nyauloso. “Kiba anasema hawezi kutoa nyimbo mpaka ile iliyotangulia imletee manufaa na iishe kabisa yaani ndio atoe nyingine. Kwahiyo huo ndo utaratibu wake, ingawa kwa upande mwingine kuna madhara. Sawa tunajua ukitoa ngoma nzuri lazima uipe time kidogo watu waenjoy lakini kwa ubaya wake ni kwamba siku hizi muziki ni ushindani unaweza kutoa nyimbo moja ni kali ukasubiri lakini akatokea mwingine akatoa nyimbo tatu zikawa nzuri zaidi, so lazima atachukua mashabiki zaidi yako.”

“So mi namshauri kama hataki kutoa official kazi kama watu wanavyohitaji, basi atoe nyimbo ziwe hata kwenye mitandano watu wazidi kufurahia muziki wake au aendelee tu na tabia yake kwa vile anajiamini, sio mbaya.”

Kwa upande wake Bonge la Nyau amesema ataachia kazi mpya baada ya Sikukuu ya Eid.

Comments

comments

You may also like ...