Header

Darassa atoa dondoo hizi muhimu kwa rappers wa kike

Baada ya kuibuka kwa wasanii wa kike wa hip hop nchini, Darassa ameamua kuwashauri ili waweze kufika mbali zaidi kimuziki. Akipiga Story na Dizzim Online, mmiliki huyo wa ngoma ya Muziki amewapongeza marapper wote wa kike na kuwataka wafanye muziki kwa kujitoa zaidi.

“Unajua huu muziki umebadilika sana, so wanatakiwa kuwa serious zaidi na wajue mashabiki wanataka nini kwenye muziki wao. Mtu kuacha kazi zake na kukusikiliza wewe ni kazi kubwa sana. Kwahiyo jitahidini kufatufa beat nzuri ambazo zitawapendeza mashabiki na kuzingatia wanachokisema pia kwenye ngoma zao na wafahamu kwamba muziki wa hip hop unapendwa sana na utaendelea kupendwa zaidi kama watatizama hayo,” amesema Darassa.

Darassa anaendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya Hasara Roho.

Comments

comments

You may also like ...