Header

Filamu ya All Eyez On Me yaingiza $27m hadi sasa

Pamoja na mastaa wakubwa wakiwemo Jada Pinkett Smith na 50 Cent kuiponda, filamu ya maisha ya marehemu Tupac Shakur, All Eyez on Me inafanya vizuri kwenye majumba ya sinema.

Filamu hiyo iliyoongozwa na Benny Boom, imekamata nafasi ya 3 kwa kuingiza dola milioni 27. Kiasi hicho ni kikubwa kulinganisha na matarajio yaliyokuwepo.

Filamu hiyo iliachia siku ya birthday Tupac, June 16 ambao rapper huyo angekuwa na miaka 46. Demetrius Shipp Jr. amecheza kama Tupac huku Kat Graham akimcheza Pinkett-Smith ambaye amesema filamu hiyo imemuumiza.

Comments

comments

You may also like ...