Header

Queen Darleen afichua kuhusu kufanya kazi nje ya Wasafi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB Queen Darleen amebainisha uhuru wake wa kufanya kazi na kampuni tofauti za muziki nje ya WCB Wasafi.

Akizungumza na Dizzim Online Queen amesema kuwa mkataka wake haumbani kufanya kazi nje ya lebo hiyo ingawa ilibainisha kikubwa ambacho angependa kufanya kama ikitokea amehitajika kufanya kazi na kampuni nyingine.

“kufanya kazi na watu wengine so far kwangu mimi sio tatizo sana kwasababu Wasafi as Wasafi ni Wasafi na nimesaini na mkataba wangu haunibani lakini kwa mimi binafsi ningependa kuwa Wasafi For Life” Amesema Queen Darleen.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Queen alishaiambia Dizzim Online kuwa mwezi wanane ndo mwezi wake rasmi wa kuanza kuachia kazi zake kama msanii anayefanya kazi chini ya usimamizi wa WCB Wasafi.

Comments

comments

You may also like ...