Header

Diamond Platnumz atoa sababu ya kuchelewa kwa ‘I miss you’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz amezungumzia ujio rasmi wa ngoma na video yake ya ‘I miss you’ na kutoa sababu za kwanini ilichelewa kutoka mbali na kuwa ilifanyika muda mrefu uliopita.

Diamond Platnumz anayeonekana katika mavazi ya miaka ya 90 hivi katika video ya kazi hiyo inayotajwa kurecordiwa miaka miwili iliyopita leo Platnumz ameimbia Dizzim Online kuwa kuvuja kwa wimbo huo ni kitu kilichomuuma sana kiasi cha kuachana nayo kwa muda na kuachia ngoma nyingine tofauti ambapo katika ujio wa ngoma yake mpya na msanii kutoka Nigeria, Tiwa Savage ameona ni vyema pia iwaendee mashabiki.

Hata hivyo Diamond Platnumz katika kutoa maelezo ya muda wa ngoma hiyo kuwa mkononi ikiwa tayari bila kuachiwa, ameongeza kuwa wimbo huu wa ‘I Miss You’ ameufanya na kushoot video yake nchini Afrika Kusini kabla msanii Harmonize hajatoka kimuziki na kuwa mkubwa kama alivyo sasa.

Comments

comments

You may also like ...