Header

Moni Centrozone asukumwa kuanzisha lebo ya muziki

Msanii wa muziki wa rap kutoka Tanzania Moni Centrozone na mmiliki wa ngoma ya ‘Sembe Dona’ ameweka wazi rasmi nini sababu za kuanzisha ‘Majengo Sokoni Music Entertainment’ iliyotambulishwa sambamba na ujio wa ngoma yake mpya ya ‘Tunaishi Nao.’

Akipiga stori na Dizzim Online Moni amesema kuwa amekuwa akikutana na wasanii wengi wenye uwezo waliomfata ili awape msaada wa japo kusikika katika kuonesha uwezo wao kimuziki hata kuitaja sababu hiyo kumsukuma kuanzisha ‘Majengo Sokoni Music Entertainment’ kama chombo kitakachotumika kuwapa nafasi wasanii wenye uwezo.

“Nimekuwa nikipata maombi mengi ya wasanii hasa wa Dodoma wakinitaka niwasaidie lakini sina kitu rasmi au mwavuli ambao naweza nikasupport watu wa Dodoma ndo maana kama ukiangalia kwenye video tumekuja na kitu kinaitwa ‘Majengo Sokoni Music Entertainment’.” Amesema Moni.

Hata hivyo Moni ameutaja ujio wake wa ngoma ya ‘Tunaishi nao’ kuwa ilimlazimu aongeze mawazo na uandishi kuhusu aina tofauti ya watu wanaotuzunguka katika jamii mbali na kuwa  ngoma hiyo iliyokuwepo kabla kutokana na tukio la utekwaji lililomtokea mwezi April mwaka huu.

Itazame kazi yake mpya hapa chini.

Comments

comments

You may also like ...