Header

Nahreel asema kitakachofanyika baada ya Bajaj

Msanii na mtayarishaji wa muziki kutoka kundi la muziki wa Navy Kenzo ‘Nahreel’ baada ya ujio wa video mpya ya wimbo wa Bajaj iliyomshirikisha Patoranking kama Navy Kenzo kutoka katika Album yao ya Above Inna Minute(AIM) ametangaza video ya kolabo nyingine itakayoshootiwa hivi karibuni.

Akizungumzia mafanikio na mapokezi ya Album hiyo Nahreel amesema kuwa kwenye album imepangwa nyimbo zitoke audio katika mfumo wa album kisha video zifuate ambapo tayari video za nyimbo nne zimetoka.

“tumetoa Morning ambayo imetoka kwenye album, tumetoka Bajaj ambayo ipo kwenye album, tumeshoot pia Bless up pia tunataka kushoot na Mr Eazi tunakutana naye kwenye show ya Kongo nadhani mwezi wa saba…tutashoot naye video kwa hiyo ilikuwa ni mipango tokea mwanzo tunatoa album tukasema video zake zitafuata na tunaweza tusishoot zote tuashoot labda tano” Amesema Nahreel alipokwa akiongea na 255 ya Clouds Fm.

Hata hivyo Nahreel anategemewa kuandaa ujio wa ngoma mpya wa msanii Anto Neosoul kutoka nchini Kenya kwakuwa tayari wimbo umesharecordiwa na Hascana ndiye director aliyechaguliwa kuongoza video ya wimbo huo.

Comments

comments

You may also like ...