Header

Prodigy wa Mobb Deep afariki Dunia

Mkali wa muziki wa Rapa na mwanakikundi cha muziki wa Hip Hop na rap cha Mobb Deep kutoka Marekani Prodigy, amefariki dunia akiwa ni mwenye umri wa miaka 42.

Mkongwe huyo alikuwa mjini Las Vegas kutumbuiza katika ziara ya ‘Art of Rap’ huku akisindikizwa na wakali wenzake Ghostface Killah, Onyx, KRS-One na Ice-T kabla ya kulazwa hospitalini kwa siku kadhaa ambapo haijabainika ni nini kimesaabisha kifo chake lakini kwa mujibu wa taarifa za awali ni kuwa amekuwa akiugulia Ugonjwa wa selimundu (sickle cell disease) tangu kuzaliwa kwake.

Prodigy enzi za uhai wake amewahi kuingia katika bifu nzito na rapa marehemu TuPac.

Prodigy na mwenzake Havoc kwa pamoja waliunda kundi hilo maarufu la Mobb Deep katika jimbo la New York kwenye miaka ya 90 ambapo waliweza kufanya vizuri zaidi na ngoma zao kama ‘Quiet Storm’ na ‘Shook Ones’.

 

Hizi ni za Tweets za mastaa kuhusu kuhusu kifo cha Prodigy.

Pia Nas kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost

🙏🏾 QB RIP King P. Prodigy 4 Ever

A post shared by Nasir Jones (@nas) on

Family. We Mobb Deep 4 Ever. RIP PRODIGY

A post shared by Nasir Jones (@nas) on

Comments

comments

You may also like ...