Header

Bright akanusha kuandikiwa na Barakah The Prince

Msanii na mkali wa ngoma ya ‘Nitunzie’ aliyomshirikisha Barakah The Prince ‘Bright’ amekanusha tetesi za kuandikiwa na Barakah The Prince.

Akikanusha hilo Bright amesema kuwa amekuwa muandishi wa kujitegemea katika nyimbo zake kisha kujitofautisha na mfumo wake wa uandishi anaoutumia Barakah.

“Barakah hana kigezo cha kusema mimi ananiandikia au watu wanaosema mimi naandikiwa na Barakah…ukiangalia kwenye kolabo yangu ya Nitunzie unaona nini ambacho kimeongelewa” kupitia ENews Alisema Bright.

Hata hivyo Bright ameongeza kuwa kutokana na uwezo wake katika uandishi wapo baadhi wanamwambia kuwa zipo ngoma ambazo anaandika vitu vikubwa kumzidi umri wake.

Comments

comments

You may also like ...