Header

Linex ataja sababu ya kuchelewa kwa video ya Kiherehere

Linex ameeleza sababu za kuchelewa kutoka kwa video ya wimbo wake Kiherere uliotoka mwanzoni mwa mwaka huu. Ameiambia Dizzim Online kuwa ratiba za show za nje ya Dar zimemkwamisha.

“Unajua tangu nitoe audio tu ya Kiherehere kuna kazi niliipata ambayo nilikuwa nafanya long show,” amesema. “Na sio kwamba nilikuwa sijaanza kabisa kushoot, hapana, nilianza nikaishia kati ikanibidi nifanye hiyo kitu,” ameongeza/

“So nawaomba mashabiki zangu waendelee kuniamini kama walivyokuwa wakiniamini zamani kwasababu ni kazi tu ndio ziliingiliana na ilinibidi nifanye kwa wakati huo mmoja.”

Comments

comments

You may also like ...