Header

Mayanga aeleza sababu za kukosekana kwa Samatta, Farid (+Video)

Kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga ameeleza sababu za kutokuwepo kwa wachezaji Mbwana Samatta pamoja na Farid Mussa katika kikosi cha  timu ya Taifa ya Tanzania kilichosafiri hii leo kuelekea katika michuano ya COSAFA inayofanyika Afrika kusini.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mayanga amesema kuwa likizo ya Mbwana Samatta ilikua tayari imemalizika hivyo alihitajika kurejea katika klabu yake ya KRC Genk huku Farid Mussa akiwa amerejea pia katika klabu yake baada ya kuombwa akaisaidie timu yake ya Tenerrife inayogombania kupanda daraja.

“Kepteni (Samatta) alikua likizo katika mawasiliano nae anamaliza likizo tarehe 27 anatakiwa awepo kule kwenye klabu yake tarehe hiyo haya mashindano tunayokwenda yako nje ya karenda ya FIFA kwaiyo tulikubaliana nae atarudi kule likizo yake ikimalizika watu walikua wanauliza kwanini ameachwa”.

“Farid vivyo hivyo tulizungumza nae alikubali lakini timu yake ipo kwenye play off games kule kwao walimuomba arudi akamilizie mechi kwa sababu wanapanda daraja, Maguli na Thomas wao likizo zao hazina tatizo kwa wachezaji wa nje hivyo wamekubali tutaenda nao”. Alisema Mayanga.

Stars imeondoka leo jioni, kushiriki michuano hiyo ya COSAFA iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika kama timu mwalikwa, Tanzania si mwanachama wa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu.

Taifa Stars imepangwa kundi A na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.

Comments

comments

You may also like ...