Header

Mchezaji wa Klabu ya Tottenham autaja wimbo anaoupenda kutoka Tanzania

Mchezaji wa soka la kulipwa wa klabu ya Tottenham ya Uingereza kutoka nchini Kenya ‘Victor Wanyama’ ameutaja wimbo anaousikiliza na kuukubali kwa sasa wa msanii kutoka Tanzania.

Akipiga stori na Sports Extra ya Clouds Fm, Wanyama amesema kuwa anao muda wa kusikiliza kazi za wasanii wa muziki na wimbo mpya wa Saida Karoli wa ‘Orugambo’ anaupenda na kuusikiliza mara kwa mara kwa kipindi hiki ambacho yupo Tanzania.

“ Nafatilia…nafatilia na nafikiria wasanii wote wanaimba vizuri so mimi uwa nasikiliza…na nimependa wimbo huu mpya wa Saida Karoli, nimeipenda sana na napenda kusikiliza” Amesema Victor Wanyama.

Hata hivyo itakumbukwa kuwa mwezi uliopita mchezaji mkongwe wa kandanda kwa Nigeria Jay Jay Okocha alipokuwa nchini Kenya alimpongeza Wanyama wa kazi nzuri na hatua kubwa aliyopiga ya kuiwakilisha Kenya na Afrika kupitia klabu ya Tottenham.

 

Msikilize Saida Karoli katika mahojiano na Dizzim Online.

Comments

comments

You may also like ...