Jun 22, 2017 at 12:08:48 AM
SHARE:

Katika tuzo za BET 2017 zitakazofanyika June 25 nchini Marekani mwaka huu ambako kutoka Afrika Mashariki tunawakilishwa na msanii Rayvanny, rapa kutoka Afrika Kusini Nasty C anayo habari njema kuhusu kolabo yake na mkali kutoka Marekani French Montana.
Kupitia ukurasa wa Instagram Nasty C ameonekana kufurahia uwepo wake huko Marekani ambapo ametoka taarifa rasmi kuhusu kufanyika kwa video ya kolabo yake na French Montana ya ngoma ya ‘Allow’ iliyotoka mwaka jana itakayoshootiwa mjini L.A.
Nasty C anayetajwa kuwa rapa mwenye umri mdogo na mwenye mafanikio kimuziki mbali na uthibitisho wa kushootiwa kwa kolabo yake hiyo pia atahudhuria tuzo za BET zitakazo fanyika mjini Los Angeles.
Nasty C- Allow ft. French Montana.