Header

Nyota Ndogo na ex wa mume wake ni kama chanda na pete

Si jambo la kawaida mwanamke kuwa rafiki na mke wa aliyekuwa mume wake. Kwa ex wa mume wa sasa wa muimbaji wa Kenya, Nyota Ndogo, hali ni tofauti. Wanawake hao ni marafiki.

“Yani wazungu wapo tafauti sana,” anasema Nyota kwenye post ya picha akiwa na mama huyo aliyekuwa mke wa mume wake. “Huyu ni aliekua mke wa mume wangu, huyu ndie mwenye wale watoto wakubwa yani wapo na wajukuu na mume wangu,” ameongeza.

“Yani huyu aliponiona mara ya kwanza alinikumbatia na kuniambia karibu katika familia, alinifunza kupika lazanya yani mwanamke mzuri sana.nae aliolewa kwengine pia yupo na watoto wakubwa uko alipoolewa @cbrandhoej you have the best mum in the world.”

Comments

comments

You may also like ...