Header

‘Kamati itatenda haki kwa kila mgombea’; Msemaji TFF

Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Alfred Lucas Mapunda amesema kuwa shirikisho haliwezi kuvunja kanuni na taratibu katika zoezi la kuhakiki majina ya Wagombea wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu mkoani Dodoma.

Akizungumza na Dizzim Online Lucas amesema kuwa, kamati ya uchaguzi ipo makini na haiwezi kuvunja sheria yoyote kwa kumpendelea au kumuonea mgombea, badala yake haki lazima itendeke kwa wote waliogombea hasa kwa wale waliofata sheria na utaratibu wa kujaza Fomu.

“Uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu, na kwa msingi huo kila hatua zinafuatwa kawaiyo TFF kwa ujumla wake lakini zaidi kamati ya uchaguzi haiwezi kukwepa kufata kanuni za uchaguzi, kamati inafata hatua moja baada ya nyingine bila kuruka hatua hata moja maana kwa kuruka hata moja tayari itakua imevunja sheria kwa msingi huo kila kanuni iliyoelekezwa kwenye fomu lazima ifuatwe”. Alisema Afisa habari huyo.

Pia Alfred Lucas amesisitiza kuwa kila mgombea atakaeondolewa katika uchaguzi huo atapewa taarifa na kutajiwa makosa yake yaliomfanya kuondolewa katika uchaguzi huo

“Fomu zote zitaangaliwa na kuchunguzwa kama mtu kajaza matusi au kashindwa kufata maelekezo ya kujaza ataambiwa na kuonyeshwa makosa yake ili kusilete changamoto yoyote wala kuleta hisia za tofauti kwa watakaochujwa”.

Kwa sasa kamati ya Uchaguzi mkuu ipo katika mchakato wa kukagua Fomu zote za wagombea tangu Juni 20 na inatarajiwa kutoa majibu ya mchujo wa awali siku ya kesho Juni 24 baada ya kukamilisha zoezi hilo. Kwa mujibu wa ripoti ya TFF jumla ya wagombea 74 ndio waliochukua na kurejesha fomu kwa nafasi zote.

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...