Header

‘Nenda Salama’ Utata kwa Nedy Music na PKP?

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mkali wa ngoma ya ‘Dozee’ Nedy Music ameachia wimbo ambao unawaacha na maswali baadhi ya mashabiki wanaofatilia muziki wake.

Nedy anayetambulika zaidi kwa kufanya kazi chini ya usimamizi wa lebo ya muziki inayomilikiwa na Ommy Dimpoz ‘PKP’ ameachia video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Nenda Salama’ na wengi kujiuliza sababu za kwanini wimbo huo haujatoka kwa kivuli cha ‘PKP’ kama ulivyo utaratibu wa kuachia ngoma zake.

Wachache bila kufatilia zaidi walidhani kile kilichodaiwa kutokwepo kwa mahusiano mazuri kati yake na Ommy Dimpoz mbali na kuwa Nedy alishaweka wazi kuwa hakuna matatizo kati yao kianweza kuwa sababu ya wimbo huo kutoka bila usimamizi wa ‘PKP’. Kwa mujibu wa ufatiliaji na upekuzi kuhusu wimbo huo ulioachiwa mtandaoni bila kivuli cha ‘PKP’ umeonekana kuwa video ya wimbo huo iliigia mtandaoni tarehe kabla ya Nedy kuingia katika mkataba na ‘PKP’ yaani 25 Dec mwaka 2014 ambapo imewekwa public Juni 20, 2017.

Kupitia Ommy Dimpoz, rasmi Nedy Music alitambulishwa kama msanii wa ‘PKP’ Mei 5 mwaka jana ambapo chini ya usimamizi huo mpaka sasa ameachia nyimbo tatu ambazo ni Usinde Mbali iliyomshirikisha Ommy Dimpoz, Rudi iliyomshirikisha Christian Bella na Dozee.

Comments

comments

You may also like ...