Header

Christian Bella asema wasanii wa bendi hawajiongezi

Christian Bella ameitaja sababu ya muziki wa dance kufifia ni wasanii wake kushindwa kujiongeza. Ameiambia Dizzim Online kuwa mazingira ya muziki wa Tanzania yamebadilika hivyo wasanii wa muziki huo wanapaswa kwendana nayo.

Amesema, “Kiukweli yaani ugonjwa mkuu ulioukuta muziki huu sijajua, lakini tujue kwamba muziki unaenda na upepo, kuna mda fulani upepo unakuwa kwenye muziki wa Taarab, muda mwingine kwenye Bongo Flava.” Ameongeza, “Lakini pia mi nafikiri muziki wa bendi watu wanatakiwa kujiongeza kwenda na wakati ndio kitu kikubwa. Haiwezekani mpaka leo we msanii wa dance unataka kufanya muziki wa 2001 au 99 huko, hilo ndio sumu ambayo mimi naiona. Wasanii wanashindwa kujiongeza na kwenda na wakati kama Malaika Band, sisi tunaenda na wakati na ndio maana ngoma zetu zinakuwa nzuri kila tunapoachia.”

Hata hivyo Malaika Band imekuwa kimya kwa muda tangu walioachia ngoma yao mwaka jana.

Comments

comments

You may also like ...