Header

Himid Mao akanusha kujiunga Yanga Sc

Nahodha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania na kiungo wa klabu ya Azam Fc Himid Mao Mkami amekanusha tetesi zinazozagaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii zinazomhusisha mchezaji huyo kuhamia klabu ya Yanga.
Himid Mao amefanya mahojiano na Dizzim Online dakika chache kabla ya kusafiri na timu ya Taifa ya Tanzania iliyoenda kushiriki michuano ya COSAFA Afrika kusini. katika mahojiano hayo Himid Mao amesema bado yeye ni mchezaji wa Azam Fc na kudai kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wake wasikiamini.
“Mashabiki wangu kwanini wanakua na hofu na mimi kuendelea kuwepo Azam msimu ujao, mimi ni mchezaji wa Azam, mimi huwa siamini tetesi mashabiki nao wasiziamini kama mimi nisivoziamini, mimi bado nipo Azam na ndio wanaonilipa mshahara mpaka leo”. Alisema Himid Mao.
Kauli hii inathibitisha kuwa taarifa zinazoendelea kuenea katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuhusiana na kiungo huyo kuondoka Azam Fc hazina ukweli wowote.

Comments

comments

You may also like ...