Header

TID amtaka Quick Rocka amlipe 20m kwa kutumia kinyemela chorus ya ‘Watasema Sana’

TID Mnyama anamtaka Quick Rocka amlipe fidia ya shilingi milioni 20 kwa kutumia chorus ya wimbo wake wa zamani, Watasema Sana kwenye wimbo wake mpya aliowashirikisha vijana wa label ya SMG, OMG. Wimbo huo ambao video yake imetoka Jumamosi hii unaitwa Watasema.

Pia amemtishia kumpeleka polisi rapper huyo.

“Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema,” TID ameandika kwenye Instaram. Ameongeza, “Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo.”

Tumemtafuta Quick Rocka kuzungumzia suala hiyo, bado hajaweza kutoa maelezo. Endelea kufuatilia habari zetu kujua jibu lake.

Comments

comments

You may also like ...