Header

Diamond Platnumz amhusisha Adele na kuchelewa kwa ngoma ya ‘I miss You’

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz amesimulia kugongana kwa wazo la uandishi wa ngoma yake ya ‘I miss You’ na wimbo wa ‘Hello’ wa Staa wa Uingereza Adele.

Akizungumzia sababu zilizochangia kuchelewa kutoka wa wimbo huo wa ‘I miss You’ Diamond amesema kuwa akiwa nchini Italia baada ya kusikiliza wimbo mkubwa wa Hello wa Adele aligundua kufanana kwa mwanzo wa ngoma hiyo na matumizi ya neno la ‘HELLO’ hali ambayo ilimpa hofu ya kuhisi kuwa atakapoachia wimbo huo ataonekana kuwa alitumia wazo la mtu.

“wakati nimeandika hii nyimbo ninayo ndani…mimi nimesafiri nimeenda Italy, mara ya kwanza nasikia ile nyimbo ya Adele ile ya Hello nilikuwa niko na meneja Sallam…nikapagawa, nikasema mbona huyu kaimba kama mimi nilivyoanza mwanzo alafu nyimbo ninayo ndani!?. Nafikiri hiyo pia ilichangia nyimbo isitoke nisije kuonekana nimemuiga huyu…kwasababu sometime idea zinagongana” Alisema Diamond Platnumz.

Hata hivyo Diamond ameitaja ngoma ya ‘I miss you’ kuwa ni ngoma ambayo iliandika kwa hisia sana ambapo wazo la wimbo huo alilipata akiwa safarini.

Wimbo wa Adele uliofanana wazo katika uandishi wa ngoma ya ‘I miss you’.

Comments

comments

You may also like ...