Header

Nay wa Mitego apangua kwa maneno Diss ya Youngkiller

Mkali wa muziki wa rap kutoka Tanzania Nay wa Mitego a.k.a True Boy ameukingia kifua kwa maneno wimbo wake wa ‘Moto’ alipokuwa akitoa majibu kuhusu wimbo wa ‘True Boya’ wa Youngkiller uliyomlenga Nay kwa kiasi kikubwa ambao pia ulitoa onyo kwa marapa wengine wenye wazo la kumdiss.

Akipiga stori na SamMisago Tv, Nay amesema kuwa amesikia jibu la diss ya wimbo wa ‘True Boya’ na kuongeza kuwa mbali na majibu hayo ya Youngkiller bado anasimama kwenye ukweli wa maneno yake kwa alichosema katika wimbo wa ‘Moto’ kwakuwa amewasilisha kile kinachosemwa na baadhi ya mashabiki na baadhi ya wadau wa muziki kwa sasa.

“mimi uwa nasimama kwenye ukweli, nazungumza kitu ambacho kipo ndo maana watu wamekuwa na imani na mimi…juu ya hili kila mtu anajua, Youngkiller biashara yake imekuwa ngumu sana…niliowachana wanatakiwa kuamka na kujua wapi wanakosea” Amesema Nay wa Mitego.

Hata hivyo Nay kuhusu kuachia wimbo wake huo ‘Moto’ uliowachana wadau na mastaa kibao huku wengine akiwataja kwa majina, amesema kuwa sababu yake kuu ya kufanya hivyo ni kutokana na mtazamo wake wa kuona kuwa asilimia kubwa ya wasanii kwa sasa wanaandaa na kuachia nyimbo za kawaida.

Comments

comments

You may also like ...